UTU UMEJAA KUTU
Ziko wapi zama za kale,nilizozisikia kule Nambale
Undugu ulikuwa kufaana,haukuwa katu kufanana
Ukarimu kwa kila mja,kusaidiana nambari moja
Mambo keshageuka,utu umejaa kutu.
Fukara wateseka,wenye navyo wana makeke
Maradhi keshavamia,wachochole hawana nia
Wamekuwa tangatanga,ombaomba jina lao
Mambo keshageuka, utu umejaa kutu
Mabwenyenye wajionyesha,wasaidiapo walalahoi
Pale mitandaoni,picha zatamba anuwai
Wanazopiga na kuposti,wakipeana yao misaada
Mambo keshageuka, utu umejaa kutu.
Spencerpenfam©2020
malenga mpole
SHARON OBANDA
SPPF

Comments
Post a Comment