KIRUSI GIZANI
Hii ni yangu barua,japo isiyo rasmi
Kubali kuipokea, uinusuru jamii
Magoti naangukia,Mola jibu langu ombi
Limetuingia Giza, kirusi korona giza
Naita tena naita, milimani kiangalia
Ewe Mungu nakwita,sikia na angalia
Duniani Kuna nta, ya uwele usosikia
Limetuingia giza,kirusi korona giza
Labda ni mwisho,wa sayari ya tatu
Dunia ina vitisho,vimejaa matu
Uwele hauna bisho,hii sayari ya watu
Limetuingia giza, kirusi korona giza
Yameshinda na uchina,wanalia Italia
Dunia haina zana,uhai kupigania
Ila tunakazana na,janga hili la Dunia
Limetuingia giza, kirusi korona giza.
Najua tuna ujuzi, wa miili kutibu
Japo uwele u wa juzi, umeshinda matabibu
Kirusi hiki kijuzi, Labda kwako tutubu
Limetuingia giza, kirusi korona giza
Spencerpenfam©2020
#sanitize
EUGENE JOSEPH
SPPF
Hii ni yangu barua,japo isiyo rasmi
Kubali kuipokea, uinusuru jamii
Magoti naangukia,Mola jibu langu ombi
Limetuingia Giza, kirusi korona giza
Naita tena naita, milimani kiangalia
Ewe Mungu nakwita,sikia na angalia
Duniani Kuna nta, ya uwele usosikia
Limetuingia giza,kirusi korona giza
Labda ni mwisho,wa sayari ya tatu
Dunia ina vitisho,vimejaa matu
Uwele hauna bisho,hii sayari ya watu
Limetuingia giza, kirusi korona giza
Yameshinda na uchina,wanalia Italia
Dunia haina zana,uhai kupigania
Ila tunakazana na,janga hili la Dunia
Limetuingia giza, kirusi korona giza.
Najua tuna ujuzi, wa miili kutibu
Japo uwele u wa juzi, umeshinda matabibu
Kirusi hiki kijuzi, Labda kwako tutubu
Limetuingia giza, kirusi korona giza
Spencerpenfam©2020
#sanitize
EUGENE JOSEPH
SPPF
Huu ndio mwanzoni..... Sppf ina washairi waliobobea
ReplyDelete