Francis Wakhu Omusula alizaliwa mnamo tarehe 18 mwezi wa januari mwaka wa 1996 katika kaunti ya Kakamega (037); kaunti ndogo ya Butere ; Kanda ya Buchenya. Yeye ni mzaliwa wa nne kwa familia ya watoto Saba. Francis alianza masomo yake ya chekechea mnamo mwaka wa elfu mbili na mbili katika shule ya msingi ya Bululwe ambapo aliufanya mtihani wake wa kitaifa wa darasa la nane huko na kuweza kunyofoa alama bora. Baada ya hapo, alijiunga na shule ya upili ya Shibanga kule Butere na kuwa mojawapo wa waanzilishi waliofuzu vyema kutoka ile shule. Baada ya hapo, Francis alikuwa na ari ya tamaa ya kuwa mwalimu. Alijiunga na Chuo kikuu Cha Mount Kenya mwaka wa 2016 septemba na kufuzu na First Class Honours katika shahada ya ualimu( Kiswahili na Historia). Pia , aliweza kupata tuzo la mwanafunzi bora wa kiume kati ya maghafali waliofuzu katika hicho chuo Cha MKU (Kitengo Cha Fadhili la serikali)
Francis aliwahifunza Shule ya akademia ya Butere Pace Junior, Shule ya upili ya Shibanga na pia shule ya wasichana ya Nyakiambi kule Nyandarua.
Francis ni mwandishi wa tungo za kifasihi na ambaye amewahi andika mashairi ya kuvutia na ya kusisimua. Hivi sasa, anaandika Riwaya yake ya 'Maisha Mzunguko' ambayo itaweza kuchapishwa kabla ya mwezi wa Agosti. Pia , anaziandika hadithi fupi ambazo zitaweza kuchapishwa na shirika la Spencerpenfam ambalo yeye ni mwanachama huko.
Francis anaitetea nafasi ya Fasihi ya Kiswahili kama malighafi ya Afrika Mashariki. Katika maongezi yake asema, " Kiswahili ni nyenzo ya umoja wa Afrika Mashariki na kwa hivo,nina jukumu la kuhakikisha kuwa nimekieneza na kukitetea daima".Hivi karibuni, shirika la Spencerpenfam litakua linatoa jarida ambapo kazi zake Francis zitajumuishwa.
Asanteni.
Limechapishwa na Kelvin
www.spencerpenfam.blogspot.com
©2020
Hongera
ReplyDeleteTunashukuru sana
DeleteNampongeza sana Mwalimu mwenza Francis kwa kazi yake nzuri
ReplyDeleteNaomba Mungu amuongoze kwa kila jambo afanyalo
Shukran
DeleteNampongeza sana Mwalimu mwenza Francis kwa kazi yake nzuri
ReplyDeleteNaomba Mungu amuongoze kwa kila jambo afanyalo
Shukran
DeleteHongera.. Kazi nzuri mnayoifanya
ReplyDeleteNaomba mungu awe nanyi