MFUMO MPYA WA ELIMU
Waanze na 'kubaliana,lisiwe jambo la baa,
Wakope bora mifano,tena iwe ya kufaa,
Wauunge wote mkono,u' mfumo wa manufaa,
Kwa washikadau wote,jambo hili la manufaa.
Kisha waupambanue,utofauti ulofaa,
Wakenya wautambue,lisiwe ni la fadhaa,
Tena walichanganue,lisije kutuhadaa
Kwa washikadau wote,jambo hili la manufaa.
Tatu walitekeleze, kisha lanze kuzagaa,
Kwa undani waleneze,tena kwa wote wakaa,
Halafu walitembeze,ili lianze kung'aa,
Kwa washikadau wote,jambo hili la manufaa.
Sifa nazo walipambe,wananchi sije kukataa,
Njema sifa zikatambe,wasiseme ni balaa,
Walobobea walumbe,bila domo kujikwaa,
Kwa washikadau wote, jambo hili la manufaa.
Mwisho natamatilia,kwa ajili ya mtalaa,
Mda wanitamatilia,yanibidi kunyamaa,
Yangu nimewaambia,kwani tuweze kupaa,
Kwa washikadau wote,jambo hili la manufaa.
Spencerpenfam©2020
Shukran,
Bwana Wakhu Francis,
SPPF

Wakhu anaweza. Ajizatiti zaidi
ReplyDeleteShukrani, tutazidi kuandika
DeleteKazi safi
ReplyDelete